Upungufu wa Maudhui ya Kiisimu katika Miongozo ya Walimu ya Kiswahili Shule za Sekondari Nchini Burundi

Authors

  • Anitha Nduwamahoro Chuo Kikuu cha Burundi
  • Zelda Elisifa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Abstract

Makala hii inachunguza upungufu wa maudhui ya kiisimu kwenye miongozo ya walimu ya Kiswahili katika shule za sekondari nchini Burundi, mifano ikimakinikiwa katika kitengo cha lugha. Data zilikusanywa kutoka katika miongozo mitatu ambayo ni Mwongozo wa Mwalimu wa Kiswahili, Kidato cha 1; Mwongozo wa Mwalimu wa Kiswahili, Kidato cha 2, na Mwongozo wa Mwalimu wa Kiswahili, Kidato cha 3. Nadharia ya Uchanganuzi wa Maudhui ilitumika kuchambua data. Matokeo yameonesha kuwa maudhui ya kiisimu katika miongozo husika yanaathiriwa na upungufu mwingi kama vile mpangilio wa mada usiofaa, fasili za dhana za kiisimu zisizo sahihi wala kamili, usosahihi wa lugha na ukosefu wa uwiano wa baadhi ya mada za kiisimu na maudhui yake. Makala hii imechangia kwa kutoa ushahidi wa kitaaluma juu ya upungufu wa miongozo husika na kuweka misingi ya maboresho ya nyenzo hizo muhimu.

http://doi.org/10.56279/jk.v89i1.7

☍ View Article Analytics

Published

2026-06-30

Issue

Section

Articles