Uchanganuzi Kilongo wa Misemo ya Kiswahili katika Harakati za Utunzaji wa Mazingira

Authors

  • Salome J. Kotira Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Misemo ni nyenzo muhimu ya mawasiliano inayobeba maarifa, maadili na mitazamo ya kijamii kuhusu masuala mbalimbali ya maisha. Katika zama hizi za mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la uharibifu wa mazingira, ambapo jamii nyingi duniani zinapambana nayo, misemo imekuwa sehemu ya mapambano hayo. Utafiti huu umechunguza namna misemo ya Kiswahili inavyotumika kuhamasisha utunzaji wa mazingira. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi wa kimaudhui wa machapisho ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram, kisha zikachambuliwa kwa kutumia Nadharia ya Uchanganuzi Kilongo ya Fairclough (1992). Matokeo ya uchambuzi yamebanisha kuwa misemo inahamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira na kuonya kuhusu athari za uharibifu wake kwa kutumia mbinu kama vile matumizi ya tamathali za semi, lugha ya amri na ukanushi. Aidha, imebainika kuwa misemo pia hutumika kwa kiasi kikubwa katika kampeni mbalimbali kama vile za upandaji miti, utunzaji wa mazingira, pamoja na kampeni za kuhamasisha utalii.

http://doi.org/10.56279/jk.v89i1.8

☍ View Article Analytics

Published

2026-09-30

Issue

Section

Articles