
Kutafuta Maana katika Ulimwengu Usiojali: Uchambuzi wa Ubwege katika Riwaya za Nagona na Mzingile za Euphrase Kezilahabi
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Ubwege ni mkondo mmojawapo unaotumiwa na waandishi wa kazi za kifasihi kueleza hali mbalimbali za maisha ya mwanadamu ulimwenguni kukosa maana. Ingawa fasihi ya ubwege ilianzia Ulaya, baadhi ya kazi za fasihi ya Kiswahili, kama vile riwaya za Euphrase Kezilahabi za Nagona (1990) na Mzingile (1991), zimedokezwa kusawiri ubwege huo (Deigner, 2019). Makala hii inachunguza jinsi ubwege ulivyojidhihirisha katika riwaya hizi kwa kuongozwa na Nadharia ya Udhanaishi. Matokeo yanaonesha kuwa Kezilahabi amesawiri ubwege kupitia wahusika wanaoishi katika hali ya suitafahamu, utupu, mateso, vifo na safari zisizo na mwisho za kutafuta ukweli. Aidha, ametumia mazingira yasiyoeleweka, ploti isiyo ya kawaida, migogoro isiyopata suluhisho na wahusika wa kiishara kuonesha jitihada za mwanadamu za kutafuta maana katika ulimwengu usiojali. Utafiti unahitimisha kuwa riwaya za Nagona na Mzingile zinadhihirisha falsafa ya ubwege kwa kuonesha kuwa utafutaji wa maana ya maisha ni safari endelevu inayokabiliwa na ukimya wa ulimwengu na kutokuwa na uhakika wa kupata majibu ya mwisho. Makala hii inachangia katika kupanua mjadala wa kifalsafa katika uhakiki wa fasihi ya Kiswahili kwa kuangazia namna Kezilahabi anavyoumba taswira ya mwanadamu katika ulimwengu wa kibwege. http://doi.org/10.56279/jk.v89i1.4