Ruwaza za Uwili Zinazojitokeza kwenye Sinonimu za Asili na za Mkopo katika Kiswahili

0 Article Views All time
0 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Ukopaji wa maneno katika lugha ni moja ya tabia za lugha. Lugha inapokopa maneno kutoka lugha mbalimbali husababisha lugha pokezi kuwa na msamiati changamani, yaani msamiati wa asili ambao hautokani na ukopaji na msamiati wa mkopo. Hali hii inapojitokeza mara nyingi husababisha lugha pokezi kuwa na sinonimu mbalimbali kwa sababu neno la asili huwa na kisawe chake kutoka neno la mkopo. Lugha inapokuwa na sinonimu zenye asili tofauti, sinonimu hizo hujenga ruwaza mbalimbali ikiwa ni pamoja na ruwaza za uwili, utatu au hata unne. Ruwaza hizo hujengwa kwenye neno moja la asili na lingine au mengine huwa ya mkopo kutoka lugha mbalimbali. Kiswahili ni moja ya lugha zenye maneno kadhaa ya mkopo kutoka lugha mbalimbali za kigeni kama vile Kiingereza, Kiarabu, Kihindi, Kiajemi na Kituruki. Kuwapo kwa maneno ya mkopo katika lugha ya Kiswahili kunaifanya lugha hiyo kuwa na msamiati changamani. Hali hii hutengeneza ruwaza mbalimbali za sinonimu za asili na za mkopo. Makala hii inajadili ruwaza za uwili zinazojitokeza kwenye sinonimu za asili na za mkopo katika lugha ya Kiswahili. Data za makala hii zimekusanywa kutoka Kamusi za Visawe (2014), Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2019) pamoja na uwandani. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Vijenzi Semantiki na Nadharia ya Matumizi. Kwa ujumla, makala hii imebaini kuwa lugha ya Kiswahili ina ruwaza za uwili tano zinazojitokeza katika sinonimu za asili na za mkopo katika Kiswahili. Ruwaza hizo ni ruwaza ya Kiingereza-Kiswahili, Kiswahili-Kiarabu, Kihindi-Kiswahili, Kiswahili-Kiajemi na Kiswahili-Kireno. http://doi.org/10.56279/jk.v89i1.6