
Ulinganishi wa Mfumo wa Sauti Katika "Lugha" za Mara Kaskazini
Kiswahili
##common.published##: February 12, 2016
272
Article Views
All time
0
Downloads
All time
0
Citations
Source: OpenAlex
Activity (views + downloads) over time
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Makala hii inahusu ulinganishi wa mfumo wa sauti katika "lugha" za Mara Kaskazini. Sauti zilizolinganishwa ni konsonanti na irabu. Ulinganishi huu umezingatia Nadharia ya Isimuhistoria na Isimulinganishi katika kuonesha uhusiano wa "lugha" zilizochunguzwa. Lengo la ulinganishi wa "lugha" hizi ni kubaini kama kuna mfanano au tofauti miongoni mwake. Matokeo yaliyotokana na data kutoka uwandani yamedhihirisha mfanano mkubwa wa "lugha" hizi za Mara Kaskazini katika mfumo wa sauti. Matokeo haya yanatushawishi tuzichukulie "lugha" hizi kama ni lahaja zinahusiana kwa karibu, na pengine zimetokana na lugha-chanzi moja na sio lugha zinazojitegemea kama zinavyotazamwa kiisimujamii.