Dhima ya Ngoma katika Tamthiliya ya Kiswahili ya Kimajaribio: Mfano kutoka Lina Ubani (1984)

234 Article Views All time
1 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Activity (views + downloads) over time

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Makala hii inachunguza dhima ya ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio. Tafiti kuhusu matumizi ya ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio zimeishia katika ngazi ya kubainisha tu pasi na kuchambua dhima zake. Kitendo cha kubainisha tu bila kuchambua dhima za ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio hakioneshi umuhimu wa kipengele hicho cha kifasihi simulizi katika kazi za fasihi andishi. Data za makala hii zimepatikana maktabani kwa kusoma tamthiliya ya Lina Ubani kisha kuchambua dhima ya ngoma. Uchambuzi wa data za makala hii umeongozwa na Nadharia ya Uamilifu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa ngoma ina dhima za kifani na kimaudhui katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio.http://doi.org/10.56279/jk.v86i1.4