RUWAZA ZA KIMOFOLOJIA ZA MAJINA YA MAHALI YA KIHAYA: MTAZAMO WA MOFOLOJIA LEKSIKA

459 Article Views All time
5884 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Activity (views + downloads) over time

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Makala haya yamechunguza ruwaza za majina ya mahali ya Kihaya 9 kwa kuchanganua vijenzimbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywakutoka katika wilaya za Muleba, Missenyi, Bukoba Vijijini na Bukoba Mjini, mkoani Kagera kwaajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksikakwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwakidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data zautafiti huu zimewasilishwa kwa kutumia majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwakwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika nakuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huoyamedhihirisha kuwa majina ya mahali yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbaliambavyo vimechanganuliwa kimofolojia. Tofauti na madai ya baadhi ya wanaisimu kuwa majinaya mahali yameundwa na mizizi au mashina tu, makala haya yamethibisha kuwa vipo vipashiomaalumu vinavyounda majina ya mahali na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia.