Nafasi ya Fasihi katika Kusawiri suala la Dini

644 Article Views All time
1312 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Activity (views + downloads) over time

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Makala haya yanatalii maana ya dini na pia, yanatalii kazi sita za fasihi jinsi zinavyolisawiri suala zima la dini kwa njia ambayo inatufanya tuhoji ni ipi nafasi ya dini kwa mwanadamu? Na je, ni kweli dini ni asasi timilifu kama ambavyo imekuwa ikichukuliwa na wanajamii? Haya ni baadhi tu ya maswali yaliyochochea uandishi wa makala haya. Hivyo basi, ili kujibu maswali hayo, makala haya yatazitalii kazi za waandishi watano ambao ni Ngugi Wa Thiong ' o, Farouk Topan, Euphrase Kezilahabi, Ebrahim Hussein na Chinua Achebe kuhusiana na jinsi walivyolisawiri suala hili la dini na jinsi linavyotuibulia maswali hayo yaliyoulizwa hapo awali. Kazi zitakazohusika katika makala haya ni The Black Hermit (Mtawa Mweusi), Things Fall Apart (Shujaa Okonkwo), Rosa Mistika, Mfalme Juha, Aliyeonja Pepo na Kwenye Ukingo wa Thim.