Maarifa ya Kiikolojia na Kijamii kutoka katika Methali za Kiswahili Zinazotaja Mimea

0 Article Views All time
0 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Methali ni kipera cha fasihi simulizi kinachopatikana katika utanzu wa semi. Methali husheheni maarifa mbalimbali yenye kuifaa jamii husika. Lengo la makala hii ni kujadili maarifa yanayopatikana katika methali za Kiswahili zinazotaja mimea ili kuelewa mchango wake kiikolojia na kijamii. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika vitabu vya methali na mazungumzo ya wanajamii. Nadharia zilizotumika katika uchambuzi wa data ni Uhakiki Ikolojia na Ontolojia ya Kibantu. Matokeo ya utafiti wa makala hii yanaonesha kwamba methali hizo hutoa maarifa mbalimbali ya kiikolojia na kijamii. Miongoni mwa matokeo hayo ni maarifa kuhusu viumbe mbalimbali kutegemeana, shughuli mbalimbali zinazofanywa na binadamu, tabia za viumbe, changamoto mbalimbali za kimazingira, utunzaji wa mazingira, utamaduni wa jamii, na uhusiano wa ikolojia na taaluma mbalimbali. Hivyo, hoja kuu ya makala hii ni kwamba methali zinazotaja mimea zinadokeza maarifa kwa jamii kuhusu mimea, utamaduni na mazingira kwa ujumla ili kufanikisha na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimazingira. http://doi.org/10.56279/jk.v88i2.4