
Itikadi ya Ardhi katika Miviga kama Mhimili wa Utunzaji Mazingira
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Mazingira na miviga ni vitu vyenye uhusiano wa karibu. Uhusiano huo unatokana na miviga kufanyika katika mazingira asilia ya jamii kwa muda na malengo ya mviga husika. Mazingira asilia kama ardhi, milima, mabonde, maziwa pamoja na chembechembe zilizopo angani kama vile jua, mwezi na nyota ni sehemu muhimu katika kufanikisha utendaji wa miviga. Mazingira hayo asilia ndiyo vitu vya mwanzo kabisa kutokea katika ulimwengu, hivyo, yana nguvu za kiutendaji zinazotumika kufanikisha mambo mengi kwa mwanadamu. Kwa hivyo, utendaji wa matambiko hufanyika katika mazingira hayo, ikiwamo ardhi, ili kujifungamanisha na nguvu za kiutendaji. Makala hii inachunguza itikadi ya ardhi katika miviga kama mhimili wa utunzaji wa mazingira huku mifano ikitoka katika matini ya ushairi wa matambiko ya Wapangwa. Data zimekusanywa kwa njia ya ushuhudiaji na mahojiano na kuchanganuliwa kwa kutumia Nadharia ya Kiroho ya Ikolojia ya Kiafrika. Matokeo yameonesha kuwa itikadi ya ardhi inayojitokeza katika tambiko imejengwa katika falsafa kwamba ardhi ni chanzo na asili ya kuwapo kwa maisha, ni utambulisho wa asilia wa jamii, imebeba misingi na kanuni zinazoongoza maisha ya wanajamii na ni chanzo cha kaniuhai. Pia, ardhi ni chanzo cha chakula na maji. Hayo yanadihirisha kuwa itikadi ya ardhi waliyonayo wanajamii, ndiyo chachu katika kutunza mazingira yao. http://doi.org/10.56279/jk.v88i2.5