Uambishaji wa Vitenzi vya Kiingereza katika Kiswahili: Mifano kutoka Mitandao ya Kijamii ya Kielektroniki

1045 Article Views All time
0 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Activity (views + downloads) over time

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Baada ya teknolojia ya habari na mawasiliano kukua, kumezuka aina nyingineya mawasiliano ambayo inawahusisha watu wenye mwelekeo mmoja kirika,kijamii na hata kitaifa kujadili masuala yao kwa urahisi na kwa gharamandogo kwa kutumia mitandao ya kijamii ya kielektroniki (MKK). Mitandao hiiinaondoa vikwazo vya kijiografia na kimiundombinu, ambapo watu kutokapande mbalimbali za dunia wanaweza kujadiliana kwa wakati mmoja au kilammoja kwa wakati wake kwa njia ya maandishi. Makala hii inachunguzanamna wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili wanavyoambisha baadhi yavitenzi vya Kiingereza kwa kutumia kanuni za sarufi ya Kiswahili katikaMKK. Data zilikusanywa kutoka katika vipindi vya redio, televisheni, facebookna twitter. Kiwango cha maneno tunachokiona ni kidogo ikilinganishwa nayale yanayozungumzwa kwa sababu si kila anayezungumza ni lazima aandikemaneno hayohayo. MKK ni uwanja mpya unaopaswa kufanyiwa utafiti kuhusumasuala mbalimbali, hususan lugha na fasihi.Dhana za msingi: unyambulishaji vitenzi, teknolojia na mawasiliano, vitenzivya Kiingereza, Kiswahili.