
Changamoto za Wanafunzi Wanaojifunza Lugha ya Kichina kama Somo kwa Wajifunzaji Wanaotumia Kiswahil Kama Lugha ya Kwanza katika Kumudu Stadi za Lugha: Mifano kutoka Shule Teule za Sekondari Nchini Tanzania
Activity (views + downloads) over time
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Kichina ni lugha mojawapo kati ya lugha za kigeni zinazofundishwa katikashule za sekondari nchini Tanzania. Katika kuboresha zoezi zima laujifunzaji na ufundishaji wa somo la kichina katika shule za sekondari,makala hii imelenga kubainisha changamoto zinazokwamisha wanafunzikuwa mahiri na namna bora ya kuweza kukabiliana na changamoto hizo.Utafiti huu uliwahusisha walimu na wajifunzaji katika shule za sekondarizinazofundisha kichina katika mkoa wa Dodoma, halmashauri ya jiji laDodoma. Shule ya sekondari Umonga, Dodoma na Kiwanja cha Ndegezilihusishwa katika utafiti huu. Aidha, mbinu za mahojiano, uchambuzimatini na ushuhudiaji zilitumika kupata data za utafiti huu. Mkabala wakitaamuli uliongoza uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Matokeo ya utafitihuu yanatarajiwa kuwasaidia watunga sera na wadau mbalimbali wa elimu,kuongoza uboreshaji wa ufundishaji wa lugha na utoaji wa rasilimali.Kimsingi matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa zipo changamotozinazokwamisha umahiri wa wajifunzaji wa Kichina kama lugha ya pilikama vile ; tofauti za kiisimu baina ya Kichina na Kiswahili, walimukutokuwa mahiri katika lugha wanayofundisha, suala la mazingira finyu yakujifunzia na upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Pia, utafitihuu utachangia katika mjadala mpana wa kitaaluma kuhusu elimu ya lughaza kigeni barani Afrika, na kupendekeza njia za uchunguzi wa siku zijazo.