Uhusiano kati ya Semantiki na Pragmatiki katika Lugha

Authors

  • Tumaini Mahendeka Taasisi ya Elimu Tanzania

Abstract

Semantiki na pragmatiki ni matawi ya isimu yanayochunguza maana ambayo yana uhusiano wa karibu kutokana na kutegemeana kwake katika kufasiri na kuelewa matumizi ya lugha. Lengo la makala hii ni kufafanua uhusiano uliopo kati ya semantiki na pragmatiki katika lugha. Data katika makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini na zilichambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa maudhui. Makala hii ilitumia Nadharia ya Maana ni Matumizi iliyoasisiwa na Ludwig Wittgenstein (1953) katika kazi yake ya Philosophical Investigation. Matokeo yanaonesha kwamba semantiki na pragmatiki zina uhusiano wa karibu kwa kuwa yote ni matawi ya isimu katika lugha ambayo yanashughulikia maana. Pia, maana za kisemantiki huibua maana za kipragmatiki na matawi yote huhawilisha ujumbe katika mawasiliano. Aidha, matawi yote huchunguza maana za ishara kwa kutumia simiotiki.

 

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v24i1.3

☍ View Article Analytics

Downloads

Published

2026-11-06