Ulinganishaji wa Kiswahili cha Bujumbura na Kiswahili cha Kivu Kimofolojia

Authors

  • Dieudonné Butoyi Chuo Kikuu cha Burundi
  • Dunlop Ochieng Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,
  • Zelda Elisifa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,

Abstract

Makala hii inalinganisha Kiswahili cha Bujumbura na Kiswahili cha Kivu ikilenga kubainisha upekee wa kimofolojia wa Kiswahili cha Bujumbura. Data zilikusanywa kutoka kwa watoataarifa thelathini (30) wa maeneo ya mji wa Bujumbura (Buyenzi) na mkoa wa Kivu Kusini (Bukavu). Mbinu za usaili na ushuhudiaji zilitumiwa na watafiti katika kukusanya data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa maumbo ya maneno ya Kiswahili cha Bujumbura na Kiswahili cha Kivu yanafanana kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, Kiswahili cha Bujumbura kina sifa mbalimbali za kipekee za kimofolojia kama vile kutotumia viambishi vya udogoshaji {bu-} na {hi-} vinavyopatikana katika Kiswahili cha Kivu. Pia, katika muundo wa vitenzi, Kiswahili cha Bujumbura hakihusishi ufupishaji wa kiwakilishi cha nafsi wala kukitumia badala ya kiambishi cha nafsi. Kuhusu kanuni za kimofosintaksia, imebainika kuwa, katika Kiswahili cha Bujumbura, uwiano wa nomino na vitenzi au nomino na vivumishi lazima usimamiwe na viambishi ngeli kutokana na ngeli ya nomino husika ilhali Kiswahili cha Kivu huweza kudondosha viambishi hivyo vyenye dhima ya kuoanisha maneno katika tungo. Kutokana na matokeo hayo, ni dhahiri kuwa Kiswahili cha Bujumbura na Kiswahili cha Kivu huwa na unasaba mkubwa wa kimofolojia.

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v24i1.4

☍ View Article Analytics

Downloads

Published

2026-11-06