Uchambuzi wa Ufupishaji wa Majina WanayopewaWasukuma Nchini Tanzania
Abstract
Utafiti huu umechambua ufupishaji wa majina wanayopewa Wasukuma kwa kuchunguza namna ufupishaji huo unavyofanyika baina yao wakati wa mawasiliano ya kila siku ili kurahisisha mawasiliano miongoni mwao. Utafiti umechambua majina ya asili ya Kisukuma na majina ya kigeni wanayopewa watoto wanapozaliwa. Uchambuzi wa majina umefanyika kwa kuzingatia dhana ya onomastikia ambayo hushughulikia majina ya mahali na majina ya watu. Utafiti huu umejikita kwenye dhana ya anthroponomastiki kwa kuangalia namna majina ya watu yanavyofupishwa wakati wa mazungumzo ya watu wa jamii za Kisukuma. Utafiti ulifanyikia katika wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, ukiongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Tahakiki Usemi. Utafiti ulihusisha jumla ya wazee wazawa 20 waliopatikana kutoka kwenye vikundi viwili vya kahawa na wanafunzi kutoka shule ya msingi Bugalama na shule ya msingi Katunguuru. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, majina wanayopewa Wasukuma hufupishwa mwanzoni, mwishoni, katikati au kutumia majina ambatani ili kurahisisha mawasiliano miongoni mwa jamii hiyo. Mapendekezo yanatolewa kwa watafiti wengine kuchunguza na kuchambua namna ufupishaji wa majina ya watu unavyofanyika kwa jamii zingine kwa kuangalia majina ya asili na majina ya kigeni.
DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v24i1.5
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Winifrida Moshi, Zelda Elisifa, Jacob Leopold

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
