Uchunguzi wa Mbinu Zinazosawiri Usihiri katika Bunilizi za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto

Authors

  • Gloria V. Kimbi Mhadhiri, Idara ya Lugha na Fasihi, Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania.

Abstract

Sihiri2 ni miongoni mwa mbinu inayotumika katika utunzi wa kazi za fasihi ya watoto, bunilizi za Kiswahili za watoto zikiwamo. Ingawa sihiri inatambulika kama nyenzo muhimu katika utunzi wa kazi za watoto, bado mbinu zinazowasilisha usihiri katika kazi za watoto hazijawekwa bayana. Suala hili limesababisha ombwe la maarifa kuhusiana na mbinu zinazowasilisha usihiri, hivyo, mbinu husika kuonekana chapwa katika kazi mbalimbali za fasihi ya watoto hususani katika bunilizi za fasihi ya Kiswahili ya watoto. Ili kupata maarifa hayo muhimu, makala hii imebainisha na kufafanua mbinu zinazowasilisha usihiri katika bunilizi teule za fasihi ya Kiswahili ya watoto ambazo ni: Sinderela (Moshi, 1995), Hadithi ya Morile (Mariki, 2004) na Hadithi za Kusisimua (Mzindakaya, 2005). Data za makala hii zilikusanywa kutoka katika bunilizi tajwa kwa njia ya usomaji na uchambuzi wa matini. Kadhalika, utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhalisiajabu katika kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data za makala hii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa usihiri katika bunilizi teule za fasihi ya Kiswahili ya watoto umewasilishwa kupitia mbinu mbalimbali kama vile: mbinu ya ndoto, utamkaji wa neno/maneno, ukiukwaji wa masharti, wimbo na mbinu ya namna au jinsi ya utendaji. Makala hii imeongeza maarifa katika fasihi kupitia bunilizi za Kiswahili za watoto kwa kupanua uga wa uelewa wa kipengele cha sihiri katika fasihi ya watoto hususani fasihi ya Kiswahili ya watoto.

 

DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v24i1.7

☍ View Article Analytics

Downloads

Published

2026-11-06