Mitindo ya Lugha Inayomsawiri Mwanamke Kiongozi katika Tamthilia za Pango (2003) na Kigogo (2016)
Abstract
Tafiti nyingi zilizofanywa kumhusu mhusika mwanamke katika tamthilia za Kiswahili zilimsawiri mwanamke kwa ujumla bila kuangazia uongozi wake. Chache zilizoshughulikia mwanamke kiongozi zimefanya hivi bila kuangazia mitindo ya lugha inayochangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi. Mitindo ya lugha ni muhimu katika kuibua maudhui ya kazi ya fasihi. Makala hii ililenga kuchanganua mitindo ya lugha inayomsawiri mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango (Wamitila, 2003) na Kigogo (Kea, 2016). Zimelengwa tamthilia hizi kwa kuwa zimeandikwa baada ya mwaka 2000 ambapo hadhi ya mwanamke kiongozi imeendelea kuimarika na jamii kuonekana kukubali uongozi wa mwanamke. Tamthilia za Pango na Kigogo ziliteuliwa kupitia mbinu ya usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zina wahusika wanawake ambao ni viongozi. Nadharia ya Udenguzi iliyoasisiwa na Derrida (1966) na kuelezwa na Ntarangwi (2004) iliteuliwa kwa ajili ya utafiti huu. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo (maudhui) ilitumiwa kukusanya data. Tamthilia teule zilisomwa na data kunukuliwa. Data ilipangwa kisha ikachanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kupitia makala hii kuwa mitindo mbalimbali ya lugha imechangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango na Kigogo.Downloads
Published
2021-04-20
Issue
Section
Articles
License
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
