Hali ya Fasihi Simulizi ya Kiswahili katika Jamii ya Sasa na Mustakabali wake
Abstract
Makala hii inawasilisha hoja kuwa fasihi simulizi ni zao la jamii na kwamba inabadilika sambamba na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni yanayotokea katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia maandiko sita yahusuyo fasihi simulizi yaliyoandikwa katika vipindi mbalimbali. Maandiko hayo ni Finnegan (1977), Mulokozi (1996 na 2017), Ngure (2003), King ' ei na Kisovi (2005) na Wamitila (2010). Maandiko haya yalituwezesha kutathmini fasihi simulizi inavyotazamwa katika vipindi mbalimbali na kuona mabadiliko katika dhana hiyo kulingana na mabadiliko ya jamii husika. Pia, data zilikusanywa kupitia utafiti wa uwandani. Data za uwandani zilikusanywa katika tanzu tatu ambazo ni ushairi simulizi, masimulizi na semi. Katika tanzu hizo tulitumia nyimbo za jadi na za kisasa, aina mbalimbali ya hadithi za kifasihi simulizi, na methali, vitendawili na misemo. Ilionekana ni muhimu kutumia tanzu mbalimbali ili kuonesha jinsi mabadiliko ya fasihi simulizi yanavyotokea. Uchambuzi na ufasiri wa data ulizingatia Nadharia ya Uhalisia, ambayo, zaidi ya mambo mengine, inabainisha kuwa kazi za fasihi husawiri maisha ya jamii husika (taz. Kearns, 1996; Ntarangwi, 2004). Uchambuzi wa data umebainisha kuwa tanzu mbalimbali za fasihi zimepitia mabadiliko mbalimbali na kwamba tanzu mpya zimeibuka na baadhi ya zamani zinaelekea kupotea.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
