Msigano wa Majina ya ' Walemavu ' katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili: Mifano kutoka Tanzania
Abstract
Walemavu wamekuwa wakilalamikia matumizi ya majina yanayowarejelea katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Jambo hili nililigundua wakati nilipokuwa ninafuatilia vipindi vya walemavu katika runinga na redio nchini Tanzania. Majina kama vile kilema, kiwete, kipofu, zeruzeru, asiyesikia na mengineyo ni baadhi ya majina ambayo wazungumzaji wamekuwa wakiyatumia kwa muda mrefu (yaani tangu zamani za kale) lakini kwa upande mwingine wanaoitwa majina hayo wamekuwa wakiyakataa. Makala haya yanachunguza msigano wa majina wanayoitwa ' walemavu ' nchini Tanzania. Vilevile, makala yatazungumzia vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo walemavu katika mawasiliano. Mambo haya yana umuhimu mkubwa wa kuzungumziwa katika makala haya kwani lengo kuu la kuwepo kwa ' lugha ' katika jamii ni mawasiliano. Pia makala haya yatatoa mapendekezo mbalimbali kuhusiana na mambo ambayo yameshughulikiwa katika utafiti huu.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
