Usimulizi Unavyoibua Dhamira katika Tamthiliya ya Kiswahili: Uchambuzi wa Tendehogo
Abstract
Makala imechambua namna usimulizi unavyoibua dhamira mbalimbali katika tamthiliya ya Tendehogo kwa kutumia mkabala wa kinaratolojia, unaochunguza namna usimulizi unavyofanyika katika simulizi. Nadharia ya Naratolojia ilitumika kuchambua sauti za usimulizi zinazojitokeza. Sauti hizi za usimulizi zimetuwezesha kujua mtazamo wa msimulizi kwamba anasimulia akiwa ndani ya simulizi, ikimaanisha kuwa anaunga mkono yanayosimuliwa; hili linabainika kwa kutumia nafsi ya kwanza ya usimulizi. Pia, msimulizi anasimulia akiwa nje ya simulizi, ikimaanisha kwamba haungi mkono masimulizi, hili linabainika kwa kutumia nafsi ya tatu ya usimulizi. Kitendo cha msimulizi kuwa ndani au nje ya simulizi katika Nadharia ya Naratolojia, kina uhusiano mkubwa na kile kinachosimuliwa. Akisimulia kwa nafsi ya kwanza (anaunga mkono na yuko ndani ya simulizi), akisimulia kwa nafsi ya pili (anaunga mkono, yuko ndani ya simulizi, na anamhusisha msomaji ili achukue hatua katika simulizi), akisimulia kwa nafsi ya tatu (haungi mkono, yaani amejitenga na yuko nje ya simulizi). Dhamira zimesawiriwa kupitia kauli za wahusika ambazo zinajidhihirisha kwa kutumia sauti za usimulizi zinazojibainisha kama nafsi ya kwanza, ya pili na ya tatu. Matokeo ya utafiti huu yameibua aina mbalimbali za dhamira zikiwamo mapenzi, usaliti na unafiki, kwa kutaja kwa uchache. Mapendekezo yanayotolewa na utafiti huu ni kufanya utafiti mwingine katika tamthiliya hii ili kuchunguza namna sauti za usimulizi zinavyoweza kuibua aina mbalimbali za utumwa katika Tendehogo.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Kioo cha Lugha

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
