Utumwa, Aibu na Historia katika Jamii za Unyamwezi
Abstract
Dhana ya utumwa inafungamana na aibu kutokana sababu mbalimbali zikiwamo, historia yake, udhalilishaji, mapokeo na matokeo hasi katika jamii. Kwa ujumla, mbali na simulizi za utumwa katika visiwa vya Zanzibar, kuna simulizi tofauti kuhusu madhila ya utumwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Baadhi yao walijishughulisha na uzalishaji mali wakati wengine waliyahama makazi yao na kuanzisha vijiji na miji katika maeneo ya mbali ili kuficha aibu hiyo. Hata hivyo, licha ya kuwapo kwa fursa anuwai kwa watumwa na vizazi vyao, bado imekuwa changamoto kuzungumzia kuhusu utumwa katika mkoa wa Tabora. Utafiti huu kuhusu utumwa, aibu na historia yake ulifanyika katika vijiji na miji ya Tabora. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa watu (vizazi vya waliokuwa watumwa pamoja na watu wazima na wazee) waliohojiwa hawakuwa tayari kuzungumza kuhusu utumwa. Wengine walisita kuhojiwa au kushiriki katika mazungumzo kuhusu utumwa kwani ni aibu kuuzungumzia utumwa ambao, kwa mujibu wa utumaduni wa Wanyamwezi, ni mwiko. Katika makala hii, aibu inatumika kueleza kwa kina ugumu wa kufanya utafiti kuhusu utumwa katika karne ya 21. Kwa kutumia simulizi za watumwa wa kike wawili, makala hii inakusudia kueleza changamoto za kusimulia masuala ya utumwa katika jamii ambayo ilikuwa vigumu kuwasilimisha watumwa ili wawe na hadhi kama wengine. Makala inatumia Nadharia za Naratolojia na Udenguzi kueleza kuhusu utumwa na aibu katika jamii.
DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v23i2.12
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Kioo cha Lugha

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
