Uhalisia wa Utumwa wa Mwanamke katika Karne ya 21: Mfano wa Tamthilia ya Jeneza Kutoka Saurabia

Authors

  • Lina Akaka Chuo Kikuu cha Daystar,

Abstract

Tatizo la utumwa hufikiriwa kuwa ni la zamani, wakati ambapo Waafrika waliuzwa kama bidhaa ili wakatumike katika mataifa ya Marekani Kaskazini na visiwa vya Karibiani. Utumwa ungalipo. Ingawa utumwa kama ule haupo kwa sasa, sura zake zinajichomoza kwa namna mbalimbali. Ingawa utumwa, uliokuwapo katika karne ya 18 na 19 hauko hai, umechukua mkondo mpya. Hivi leo wanawake wa Kiafrika huenda katika nchi za Mashariki ya Kati na Eneo la Ghuba kwa hiari yao tofauti na wanawake waliopelekwa kwa nguvu. Hata hivyo, wote hatima yao ni moja wote huishia kuwa watumwa. Hali hii na nyinginezo za kiutumwa zimewavutia wanafasihi kutumia jukwaa la fasihi kuakisi suala hili katika kazi zao. Mtafiti aliiteua kimakusudi tamthilia ya Jeneza Kutoka Saurabia iliyoandikwa na Wa Mberia (2025) ili kuchunguza namna mwanamke wa anavyotumikishwa katika karne ya 21. Mkabala wa Bales (2012) wa haki za binadamu na utandawazi uliongoza utafiti huu. Makala inatumia tamthilia ya Jeneza Kutoka Saurabia kuchunguza tajiriba za mwanamke katika utumwa pamoja na madhila yake katika karne ya 21, hususani katika mataifa ya Mashariki ya Kati. Makala hii, pamoja na mambo mengine, inaonesha kuwa utumwa bado unaendelea na wanawake, kwa kiasi kikubwa, wamekuwa wahanga wa mfumo huu dhalimu.

☍ View Article Analytics

Downloads

Published

2026-03-20