Taswira za Bahari katika Riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934)
Abstract
Simulizi za watumwa zinapatikana katika vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na riwaya ya James Mbotela iitwayo Uhuru wa Watumwa (1934), ambayo imesheheni nduni anuwai za kifani na kimaudhui. Miongoni mwa nduni hizo ni taswira za bahari. Taswira za bahari hutumiwa na wasimulizi au waandishi ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa. Makala hii inajadili taswira za bahari katika riwaya ya Uhuru wa Watumwa pamoja na dhima zake. Riwaya hii imeteuliwa kwa makusudi kwa sababu ndiyo riwaya pekee ya Kiswahili inayozungumzia utumwa kwa kina. Makala imeongozwa na Nadharia ya Udenguzi ya Jacques Derrida. Data zimekusanywa kwa kufanya usomaji makini wa riwaya hiyo. Matokeo yanaonesha kwamba riwaya hii imeichora bahari katika taswira mbalimbali. Baadhi ya taswira hizo zinakinzana lakini zinajengana na zinakamilishana katika simulizi husika. Miongoni mwake ni bahari kuashiria usalama na pia hatari au kifo, bahari kuashiria uhuru na utumwa, bahari kuashiria muungano na utengano, na kadhalika. Vilevile, zipo taswira za bahari ambazo hazioneshi jozi zenye ukinzani. Makala imebaini dhima kadhaa zinazotokana na kutumia taswira za bahari. Baadhi ya dhima hizo ni kuonesha athari za biashara ya watumwa, kubaini mchango wa watumwa katika maendeleo ya uchumi duniani, kujenga uelewa wa msomaji kuhusu biashara ya watumwa, kuibua hisia kwa msomaji, na kusawiri mandhari ya biashara ya watumwa.
DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v23i2.7
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Kioo cha Lugha

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
