
Dhima za Motifu “Paa” katika Riwaya ya Nagona (1990) na Diwani ya Dhifa (2022)
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Makala hii imechunguza dhima za motifu “paa” katika riwaya ya Nagona (Kezilahabi, 1990) na diwani ya Dhifa (Kezilahabi, 2022). Lengo kuu la makala hii ni kufafanua dhima mbalimbali za motifu “paa” katika kazi tajwa na jinsi zinavyoibua motifu katika kuendeleza falsafa ya maisha. Data za makala hii zimekusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini kutoka maktabani. Mjadala wa matokeo ya makala uliongozwa na Nadharia ya Mchomozo. Matokeo ya makala hii yameonesha kwamba mwandishi Kezilahabi ametumia motifu “paa” kama mtindo wa kuwasilisha mawazo ya kuendeleza falsafa ya maisha kwa kufanya ukiushi wa kisemantiki akitumia motifu “paa” katika riwaya ya Nagona kama motifu kuu inayosisitiza kuhusu suala la maisha kwa kuyalinganisha maisha ya binadamu na sifa za mnyama “paa”. Hivyo, neno “paa” limetumika kama motifu pofu kwa kuchanganya dhana dhahania za neno “paa” katika diwani ya Dhifa kwa lengo la kuendeleza falsafa ya maisha. DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v24i1.6