About the Journal

MULIKA ni jarida la taaluma ya Lugha na Fasihi ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. Kutokana na mahitaji kwa baadhi ya watumiaji wa Kiswahili katika njanja nyingine, muda si mrefu jarida hili litaanza kupokea makala yaliyoandikwa kwa Kiswahili lakini yanahusu nyanja nyingine nje ya Lugha na Fasihi ya Kiswahili. MULIKA limeendelea kuwa daraja kati ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika shule za Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki na kwingineko. Jarida linapatikana katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa anwani ifuatayo: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj

MULIKA ni jarida la kitaaluma linalopitia makala zake kwa mfumo wa Peer- Review na linalopatikana bure mkondoni (Open Access) likichapishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Makala zote zinapatikana bure mkondoni chini ya leseni ya Creative Commons Attribution (CC BY

Ada za Uchakataji wa Makala (APCs):

MULIKA haitozi ada yoyote kwa ajili ya uwasilishaji, uchakataji, au uchapishaji wa makala.

Maudhui na Mawanda

MULIKA ni jarida la kimataifa linalochapishwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI). Jarida linachapisha makala zinazohusu lugha na fasihi ya Kiswahili. Vilevile, jarida linahamasisha mijadala na mapitio, hususani katika masuala ya sasa yanayohusiana na lugha na fasihi ya Kiswahili. Tungo fupi za masimulizi na ushairi zinakaribishwa pia. Jarida hili limekuwa likichapisha mara moja kwa mwaka, lakini kuanzia mwaka 2021 lilianza kuchapishwa mara mbili kwa mwaka.