Jinsi ya Kuthibitisha na Kuchanganua Viambajengo na Muundo wa Virai

3192 Article Views All time
4533 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Activity (views + downloads) over time

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Makala hii inafafanua vigezo vya kubainisha viambajengo katika Kiswahili. Vigezo hivyo ni (a) ubadili, (b) usogezaji, (c) majibu mafupi na udodoshaji, na (d) uambatishaji. Vyote hutumika sana kama njia jarabati za kutambua mipaka ya virai na viambajengo katika lugha mbalimbali duniani (Aarts, 2001; Carnie, 2012; Sportiche, Koopman, & Stabler, 2014; Haegeman, 2006). Umuhimu na matumizi ya vigezo hivyo unatolewa mfano kwa kuchunguza muundo wa sentensi, virai vitenzi vyenye yambwa mbili, na tungo tata. Matumizi ya mujarabu huu wa viambajengo ni nyenzo muhimu katika kutafiti lugha kwa mikabala yote. Ni mfano bora wa utafiti wa kisayansi ambao ni jarabati.