
Uchunguzi wa Mandhari katika Ujenzi wa Usaliti
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Makala hii inashughulikia mandhari katika ujenzi wa usaliti katika diwani ya Wasakatonge ya Muhammed Seif Khatib ambayo ilisomwa na watafiti na mandhari zote zilizosawiri usaliti kudondolewa kwa kuzingatia lengo la makala, yaani kuchambua jinsi mandhari zinavyojenga usaliti katika diwani teule. Mandhari zilizotumiwa na mwandishi kujenga usaliti katika diwani teule ni pamoja na Afrika, ufukweni, sehemu za ibada, ikuluni na hospitalini. Uwasilishaji na uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia. Mbinu kuu ya ukusanyaji wa data ilikuwa usomaji makini na uchanganuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya kitaamuli. Matokeo yanaonesha kuwa mandhari zinapotumiwa kwa ustadi mkubwa huunda usaliti kama tendo linalofichwa ndani ya hisani, tendo linalokumbatiwa katika kivuli cha uongozi, tendo linalotumika kutekeleza mauaji, tendo lililofichwa ndani ya mwamvuli wa dini, na tendo linalotumika kuendeleza matabaka. Makala hii imeongeza maarifa katika fasihi kupitia ushairi wa Kiswahili kwa kupanua uga wa uelewa wa kipengele cha mandhari katika kazi za ushairi kama ilivyo katika tanzu nyingine za riwaya, tamthiliya na hadithi fupi. DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t2.9