
Utumwa wa Kimaandishi na Kupuuzwa kwa Turathi Simulizi za Mwafrika
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Dhana ya utumwa imezoeleka kama hali ya mtu kumilikiwa na kutumikishwa bila malipo. Hata hivyo, mtu anaweza kuwa katika utumwa wa kutawaliwa kiakili ambao haung'amuliki kirahisi kwani haudhihirishi mmiliki wala mmilikiwa. Kutokana na mfumo wa elimu ya Kimagharibi, Waafrika wameingizwa katika utumwa wa kimaandishi—aina ya kifungo cha kiakili kinachowafanya wafikiri na kupima uhalali wa maarifa kwa mizani ya ukuu wa maandishi . Mizani hiyo inayapa maandishi hadhi ya juu na kuwa kipimo cha maarifa, huku maarifa yasiyoandikwa yakionekana kuwa duni, yasiyo na uthibitisho, wala yasiyofaa kuingizwa katika mijadala ya kisayansi na kuwa kipimio cha kuelimika. Kutokana na hali hiyo, makala hii inatumia uga wa ukalimani wa lugha ya mizimu kuhoji mtazamo wa kutukuza maandishi. Utafiti huu ulifanyika mkoani Mwanza, Geita, Shinyanga, na Simiyu. Data zikikusanywa kupitia uchambuzi wa maandiko na usaili nusufunge na kuchambuliwa kimada kwa kuongozwa na nadharia za Ukuu wa Afrika, Mifumo ya Maarifa Asilia, na Ufasiri wa Kitamaduni. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa ukalimani wa lugha ya mizimu una nduni zote za ukalimani wa kisasa. Hivyo, ni ukalimani kama ukalimani mwingine. Kwa kuzingatia matokeo haya, makala hii inawashajiisha wanazuoni wa Kiafrika wabebe jukumu la kuuelimisha ulimwengu kuhusu turathi zao simulizi. DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t2.2