Uundaji wa Maneno ya Kiswahili katika Mawasiliano Mahalia

0 Article Views All time
0 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Uundaji wa maneno hulenga kukidhi mawasiliano kufuatia kujitokeza kwa mapengo ya mawasiliano, aghalabu, yanayosababishwa na kuzuka kwa vitu vipya au kukutana kwa makundi lugha mawili au zaidi yanayohitaji kuwasiliana na kuelewana. Makala hii inahusu uundaji wa maneno ya Kiswahili pale jamiilugha za Kundi F30, ambazo ni Wanyiramba (F31), Wanyaturu (F32) na Warangi (F33), zinapowasiliana kwa Kiswahili kwa lengo la kukidhi mawasiliano. Makala hii imeshughulikia malengo mawili ambayo ni kubainisha maneno ya Kiswahili yanayoundwa katika jamiilugha za Kundi F30 na kufafanua mbinu zinazotumika kuunda maneno hayo. Nadharia ya Usilimishaji ilitumika katika uchambuzi na mjadala wa matokeo. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni usaili na uchambuzi matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, pale wazungumzaji wa lugha mahususi za Kundi F30 wanapowasiliana wao kwa wao, hutumia maneno ya asili kutaja majina hayo, lakini wanapowasiliana kwa Kiswahili, hutumia maneno ya Kiswahili yanayofahamika ndani ya kundi hilo pana. Imeonekana zaidi kuwa maneno hayo huundwa kwa kutumia kanuni nne ambazo ni unasibu, utohoaji, uhamishaji na ukarabati-maana. Kufuatia matokeo hayo, makala hii inapendekeza kwamba maneno ya Kiswahili mahalia yakusanywe na kutambuliwa kwa kuingizwa katika kamusi mahususi za Kiswahili ili jamii pana ya Waswahili iweze kunufaika nayo. DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t2.3