
Sababu za Kuibuka kwa Uchapishaji-binafsi wa Kazi za Fasihi Andishi ya Kiswahili Nchini Tanzania
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Makala hii inakusudia kubainisha sababu za kuibuka kwa uchapishaji-binafsi wa kazi za fasihi andishi ya Kiswahili nchini Tanzania. Data za utafiti huu zilikusanywa uwandani kwa njia ya usaili kutoka kwa wadau mbalimbali wa uchapishaji. Utafiti uliozalisha makala hii uliongozwa na Nadharia ya Msambao wa Uvumbuzi iliyoasisiwa na Everett Rodgers (2003). Aidha, makala hii imetumia mkabala wa kitaamuli katika uchambuzi na uwasilishaji wa data. Kufanyika kwa utafiti wa makala hii kulichochewa na kuibuka na kutamalaki kwa uchapishaji-binafsi wa kazi za fasihi andishi ya Kiswahili ilhali uchapishaji wa kijadi wa kazi hizo ulioaminiwa na kutumika kwa muda mrefu ukiendelea kutumika. Makala hii imemaizi kuwa uchapishaji-binafsi wa kazi za fasihi andishi ya Kiswahili umeibuka na kushamiri katika karne ya 21 kutokana na sababu zifuatazo: wachapishaji kukabiliwa na changamoto za kiuchumi, kutozingatia taratibu za kimkataba, kuteua miswada ya kuchapisha kwa kuzingatia umaarufu wa majina ya waandishi; uchache wa mashirika ya uchapishaji; waandishi kukatishwa tamaa na mlolongo mgumu wa kiuchapishaji, kuombwa au kutengenezewa mazingira ya kuombwa rushwa, kukwepa shinikizo la wachapishaji la kubadili fani na maudhui ya kazi, na kusuasua kwa soko la vitabu vya fasihi nchini Tanzania. DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t2.5