Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili

0 Article Views All time
0 Downloads All time
0 Citations Source: OpenAlex

Citations by year

No citation data available yet.

Abstract

Wahusika ni kipengele muhimu cha kazi yoyote ya fasihi. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba ujitokezaji wa vipengele vingine vya msingi vya fani na maudhui katika fasihi hutegemea sana namna ambavyo mwanafasihi amewaumba wahusika wake. Makala imetumia riwaya teule tatu ambazo ni Nagona, na Mzingile za Euphrase Kezilahabi na Ziraili na Zirani ya William Mkufya. Kwa hiyo, makala imejikita kuwabainisha wahusika wa kivisasili kwa kuzielezea sifa zao za msingi zinazowatofautisha na wahusika wasio wa kivisasili. Wahusika wa kivisasili waliobainishwa ni pamoja na Kakulu, Mimi, Kizee, Ziraili, Zirani na Kinjeketile Ngwale. Aidha, makala imejadili athari ya wahusika hao katika riwaya teule. Kwa kutumia Nadharia ya Uheminitiki, tumebaini athari anuwai. Mathalani, wahusika wa kivisasili waliotumika katika riwaya wamewezesha urithishaji wa amali za kiutamaduni na uhistorishaji. Pia, wahusika hawa wana athari ya uunganishaji wa ujadi na usasa. Vilevile, wanawezesha utambulishaji wa jamii husika. DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t2.6