
Urudiaji wa Kisufi na Motifu kama Mtindo Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi
Citations by year
No citation data available yet.
Abstract
Makala hii inashughulikia aina na mchango wa urudiaji wa kisufi na motifu katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Urudiaji wa kisufi na motifu mbalimbali vimejitokeza kwa viwango mbalimbali katika utungo huu. Vipengele hivyo ndivyo misingi ya fani na maudhui katika utenzi huu. Licha ya kazi na umuhimu wa vipengele hivyo kuchunguzwa sana katika tenzi za Kiswahili, kwa uelewa wetu, hakuna uhakiki wa kina uliofanywa kuvihusu kama mitindo katika utenzi. Hivyo, lengo la makala hii ni kuhakiki kwa kina urudiaji wa kisufi na motifu kama mitindo iliyofanikisha fani na maudhui katika utenzi. Tumegundua kuwa matumizi ya mtindo wa urudiaji wa kisufi, motifu na vipengele vyake ndiyo msingi na kiini cha fani, maudhui, na maana katika utenzi. Nadharia ya Umitindo ya Geoffrey Leech (1969) ndiyo iliyotumika kwani inasaidia kuhakiki na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi kwa sababu uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hauwezi kujisimamia. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani na ulitumia mbinu ya usomaji matini. Utenzi tajwa uliteuliwa kimakusudi na data zimewasilishwa kimaelezo. Imebainika kuwa mtunzi ameonesha matumizi ya usufi kupitia motifu ya safari, ndege, na mwanga. Urudiaji huu wa kisufi unachangia uendelezaji wa dhamira ya kidini, toba, siku ya kiyama, wahusika, maudhui, na kuleta mwangwi wa kidhamira na usisitizaji. DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na44t2.8