Biashara ya Utumwa Mashariki mwa Congo na Athari zake katika Lugha ya Kiswahili
Abstract
Kama ilivyo kwa viumbe vilivyo hai, lugha inapitia kwenye nyakati tatu muhimu: kuzaliwa, kukua na kufa. Kila wakati unatokana na sababu zake ambazo, mara nyingi, hazihusiki moja kwa moja na lugha yenyewe. Baadhi ya sababu hizi zinaambatana na mazingira ya eneo ambamo lugha inatumiwa: historia, uchumi, teknolojia, saikolojia, mawasiliano na lugha za maeneo mapya. Kuwapo kwa biashara ya watumwa kati ya Afrika Mashariki na Afrika ya Kati ni mojawapo ya njia zilizochangia kuingiza Kiswahili kwenye mikoa ya Mashariki mwa Congo. Wakaaji wa mikoa hii huzungumza kwa kiwango kikubwa sana lugha za Kibantu. Hali hii inaeleza urahisi wa maingiliano ya Kiswahili, kwa upande mmoja, na lugha za maeneno haya, kwa upande mwigine. Lengo la makala hii siyo kuelezea historia ya biashara ya watumwa katika maeneo yaliyotajwa hapo juu, bali ni kuonesha ni kwa namna gani lugha ya Kiswahili iliathirika kutokana na kuingizwa kwake nchini Congo. Kwa hiyo, makala inatilia mkazo wa pekee katika kutoa baadhi ya athari katika fonolojia, mofolojia, leksikolojia na semantiki ikilinganisha lahaja mbili hizi za Kiswahili: Kiswahili cha Afrika Mashariki na kile cha nchi ya Congo.
DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v23i2.1
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Kioo cha Lugha

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
