Makovu ya Kisaikolojia ya Utumwa katika Jamii za Watanzania: Historia, Masimulizi na Tajiriba
Abstract
Makala hii inachunguza makovu ya kisaikolojia ya utumwa kwa jamii za Kitanzania kwa kutumia masimulizi ya kihistoria, simulizi za kifamilia na urithi wa kitamaduni kama vyanzo vya msingi vya uelewa wa pamoja wa kihistoria. Kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa kimaudhui, makala data zimechambuliwa kutoka katika maandiko ya kihistoria, nyaraka za makavazi na simulizi za watu binafsi kuhusu utumwa. Vyanzo hivi vilitumiwa kubaini mada kuu zinazojirudia kama vile fadhaa ya kihistoria, urithishaji wa maumivu ya kihisia, udhalilishaji wa utu na ustahimilivu wa kijamii. Makala hii imeongozwa na nadharia tatu ambazo ni Nadharia ya Utambulisho wa Kijamii, Nadharia ya Kumbukumbu ya Kihistoria na Nadharia ya Fadhaa ya Kizazi. Nadharia ya Utambulisho wa Kijamii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa athari za kisaikolojia za utumwa bado zinaendelea kudhihirika katika jamii za Kitanzania kupitia msongo wa mawazo, huzuni ya muda mrefu, hisia za kutengwa kijamii na mkanganyiko wa utambulisho. Hata hivyo, jamii hizi zimeonesha ustahimilivu mkubwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo, zikiwamo masimulizi ya kimapokeo, imani za kidini, makumbusho na sherehe za kitamaduni kama njia za uponyaji wa pamoja na ujenzi wa utambulisho chanya.
DOI: https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v23i2.3
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Kioo cha Lugha

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors who publish in Kioo cha Lugha retain the copyright to their work and grant the University of Dar es Salaam a non-exclusive license to publish, reproduce, and distribute the article.
This article is published under the Creative Commons Attribution 4.0 International (CC BY 4.0) License, which permits unrestricted use, distribution, adaptation, and reproduction in any medium, provided the original work is properly cited.
